NDANI YAKE nimeongelea pia mazingira ya wazazi wasioishi pamoja au wale waliotengana, nani akae na mtoto, baba au mama. bei ni alfu kumi tu.
Wednesday, July 24, 2013
Tuesday, July 9, 2013
Sunday, July 7, 2013
HAKI KATI YA MME NA MKE KATIKA NDOA
KUJUA haki kati ya mme na mke, haki ya mjane katika mirathi, wajibu wa baba wa nyumba, wosia sahihi kisheria, ugawaji mirathi kisheria, haki kwa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa/mtoto wa kambo, na mambo mengi yanayofanana na hayo tafuta kitabu hicho hapo juu. kinapatikana bookshop karibia zote Tanzania, utakikutak ama kilivyo hapo kwenye picha. kwa mawasiliano piga 0767 154141. karibuni sana.
SHERIA YA NDOA, MIRATHI, WOSIA,WATOTO WA KAMBO N.K ALFU 15,000/= TU.
MIAKA minne(4) iliyopita nilitembelea maeneo ya vijijini sana. kuna watoto wanapata tabu sana, wengi wao wanateseka kwasababu wazazi wao hasa akina baba wamewatelekeza, mama anawalea peke yao. pia kutengena kwa wazazi kunahatarisha ustawi bora wa watoto. Mungu anakataa kuachana kwa wanandoa, bora kusameheana kuliko kutengana na kuharibu maisha/maslahi ya watoto wenu. ukisoma kitabu hicho hapo juu utapata kila kitu kuhusu watoto wa kambo, haki kati ya mke na mme katika ndoa, kugawa mirathi kisheria, haki ya mjane kisheria na mambo mengine mengi yanayofanana na hayo. kitabu hiki kinapatikana Tanzania nzima, kwa mawasiliano piga 0767 154141. karibuni sana.
AJIRA HATARISHI KWA WATOTO NA SHERIA TANZANIA
Kitabu hiki hapa juu cha Sheria kwa Kiswahili, pamoja na mambo mengine, kimeelezea juu ya marufuku ya ajira hatarishi kwa watoto. Sheria ya Watoto Namba 21 ya 2009 pamoja na Sheria ya Ajira na mahusiano kazini hapa Tanzania, zinaeleza kuwa, ni marufuku kwa mtu yeyote kumfanyisha mtoto kazi hatarishi au zile zinazovurugha maslahi yake bora.
Mtoto ni nani? Mtoto ni mtu yeyote aliyepo chini ya miaka 18. pamoja na kwamba inaruhusiwa kumwajiri mtoto wa miaka chini ya 18 lakini si chini ya 14 kwa kazi nyepesi tu au zile zinazohusisha mafunzo, ni marufuku mtoto huyo kufanya kazi za usiku wa kuanzia saa mbili usiku na kuendelea. Inaelekeza kuwa, mtoto ana haki ya kufanya kazi, lakini zile zinazohatarisha ustawi bora wa mtoto kama vile kazi za viwandani, migodini, magari ya masafa marefu, kwenye meli, kwenye kemikali, baa na kumbi za starehe na maeneo yanayoweza kuharibu tabia yake n.k ni marufuku. hata hivyo, kazi za melini na migodini, viwandani n.k kama atakuwa anafanya kama moja ya mafunzo yake, pengine ni mwanafunzi na anafanya mafunzo kwa vitendo, inaruhusiwa; isipokuwa, sheria inataka uangalizi wa karibu kabisa wa mtoto huyo aliyepo mafunzoni uwepo. ni marufuku kumfanyisha mtoto au kumweka katika mazingira yatakayohatarisha ustawi bora wa mtoti, iwe kiafya, kielimu, kitabia n.k
hapa Tanzania wapo watoto wengi tu wanafanya kazi migodini, kwenye mabaa na kumbi za starehe. ukisoma kitabu hicho hapo juu utajua haya yote. kwa Arusha kinapatikana KASE Stores Bomani street karibu ELCT building, Dar es salaam fika imalaseko supermarket posta na bookshop karibia zote kubwa. mwanza fika serengeti bookshop, victoria bookshop, Bookpoint bookshop na Gunda bookshop. kahaa utakipata pale royal supermarket na stationaries stand kuu ya mabasi, moshi utapata bookshop zote za pale mjini, iringa na mbeya kitafika mwezi ujao. kwa mawasiliano zaidi piga 0767 154141. karibuni sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)